Monday, April 28, 2014

TRAFFIC RULE CHANGES

COMMUNITY MEMBERS ARE REQUESTED TO TAKE CAUTION WITH THE NEW TRAFFIC RULE CHANGES ON SAMORA AVE AND SOKOINE DR FROM TODAY ONWARDS.

DETAILS ON JAMAT NOTICE BOARD.



Mabadiliko ya Matumizi ya Barabara za Samora na Sokoine

Umma unatangaziwa mabadiliko ya matumizi ya barabara za Samora na Sokoine kuanzia Jumatatu tarehe 28/04/2014. Mabadiliko hayo ni kwa mujibu wa kurahisisha mzunguko wa magari katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Barabara  ya Samora :
Muelekeo mmoja (Ocean Road Hospital -> Clock Tower)
Kuanzia mzunguko wa geti la kuingia Hospitali ya "Ocean Road" makutano na mtaa wa Luthuli katika barabara hii kupitia mzunguko wa Askari (Askari Monument) mpaka mzunguko wa Mnara wa Saa (Clock Tower) ; barabara hii itatumika kwa Kuelekea Mnara wa Saa tu njia zote mbili.

Barabara ya Sokoine:
Muelekeo mmoja (Central Police -> Luthuli Street)
Kuanzia Central Police (Stesheni) katika barabara hii kuelekea Posta ya zamani mpaka makutano na barabara ya Luthuli (Karimjee Hall) barabara hii itatumika kwa muelekeo huo tu. Hii ni pamoja na sehemu ya barabara ya Kivukoni toka makutano  Kivukoni na Mkwepu mpaka Kivukoni na Azikiwe.
Aidha barabara viungo kati ya Samora na Sokoine zitaendelea kutumika kama kawaida isipokuwa barabara ya Bridge itakuwa ni muelekeo wa Samora tu kutokea Sokoine na barabara ya Morogoro itatumika mpaka makutano na Mansfield tu.